WILSON KOLINA ELISHA

WILSON KOLINA ELISHA

BLOG HII NI MUHIMU KWA JAMII KUTOKANA NA KUJIKITA KATIKA KUANDIKA HABARI TOFAUTI ZA UHAKIKA NA ZILIZOFANYIWA UCHAMBUZI WA KINA...........

Wednesday, May 16, 2018

SERIKALI MKOANI MWANZA YATOA TAHADHALI YA EBOLA



MKUU WA MKOA WA MWANZA JOHN MONGELLA AMESEMA  KUWA MKOA WA MWANZA NI KITOVU CHA BIASHARA
AMBAPO MPAKA  SASA  UGONJWA HATARI WA EBOLA  UMELIPUKA NCHI JIRANI YA DRC CONGO NA
KUSABABISHA WAGONJWA 21 WENYE DALILI ZA HOMA NA KUTOKWA DAMU KURIPOTIWA  NA WATU 17 KUFARIKI DUNIA.



BASATA WATAKIWA KUDHIBITI KAZI ZA WASANII HAWA........



Baraza la Sanaa Tanzania BASATA
limeombwa kudhibiti  kazi za sanaa za
maonesho zikiwemo FILAMU   ambazo
zinatolewa na vikundi vya wasanii nchini ambazo  zitakuwa zinakiuka  maadili ya kitanzania jambo linalo changia  mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii.

Mwalimu wa  sanaa Peter Samwel Achimwene wa kikundi cha sanaa cha Mpanda
Chombo cha jijini Mwanza 
amewataka  wazazi na walezi kutambua kuwa sanaa ni  kazi kama zilivyo kazi nyingine na kwmba pamoja
na kuwepo kwa vikundi vingi vya wasanii nchini lakini bado kazi zao nyingi
hazijajikita katika kuielimisha jamii kwa kufuata tamaduni za Kitanzania.


Friday, April 20, 2018

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MWANZA LATOA ELIMU KWA WADAU


Kutokuwepo kwa miundombinu rafiki ,Ujenzi  holela katika vilima na makazi katika maeneo yasiyozingatia sheria za  mipango miji katika jiji la Mwanza  kumetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia Jeshi la zima moto na uokoaji kushindwa kufanikiwa pindi majanga ya moto yanapotokea.

Friday, April 13, 2018

Save changesWATANO WASHIKILIWA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA KWA MAUAJI


Watu watano wakiwemo waganga wawili wa kienyeji  wanashikiliwa na kamati ya ulinzi na usalama wilayani Misungwi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kujihusisha na mtandao wa mauaji ya wanawake wanane kwa kuwakata mapanga kuwanyofoa viungo vya sehemu za siri  na matiti na kuuza kwa waganga wa kienyeji kwa imani za kishirikina.

Monday, April 9, 2018

JUMUIYA YA WAZAZI NYAMAGANA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAZINGIRA

Jumuiya ya wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza itaendelea kushirikiana na wadau wa mazingira katika kuhakikisha utunzaji na uboreshaji wa mazingira unakidhi matakwa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuhimiza upandaji  miti na utunzaji na utunzaji wake.

Sunday, April 8, 2018

KILIMO CHA MTAMA KUOKOA BAA LA NJAA KWA KAYA KANDA YA ZIWA

Ongezeko la uhaba wa chakula na umaskini kwa baadhi ya kaya za mikoa ya kanda ya ziwa unatokana na wakulima kutofikiwa na elimu ya kilimo kinachostahimili ukame na chenye tija.

Wakulima wametakiwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa kilimo kwa kujikita katika kulima zao la Mtama badala ya zao la mahindi linalotegemewa zaidi kwa chakula ili kukabiliana na balaa la njaa kwa baadhi ya kaya za mikoa ya kanda ya ziwa.

 Mkoa wa Mwanza ni moja ya mikoa ambayo inapata mvua chini ya wastani milimita 750 kwa Mwaka ambayo inafaa kwa kilimo cha mahindi hali inayosababisha uhaba wa chakula wa kaya kutokana na mabadiliko ya tabia  nchi.