Katikati ni Rais wa ALGETA, Mhandisi Ezekiel Kunyaranyara , kushoto ni Makamu wa Rais, Mhandisi Gerald Matindi na kulia ni Katibu Mkuu wa ALGETA, Mhandisi Lusekelo Mwakyami. |
WAHANDISI 350 wa
Halmashauri kutoka Mikoa 25 nchini wanachama wa chama cha wahandisi wa serikali za mitaa Tanzania ( Association of Local Government
Engineers Tanzania) ALGETA wanakutana jijini Mwanza kwa siku mbili
kujadili utoaji bora wa huduma kwa jamii.
Akizungumza na waandishi
wa habari jijini Mwanza, Rais wa ALGETA
nchini, Mhandisi Ezekiel Kunyaranyara alisema kuwa mkutano huo wa mwaka wa
wahandisi wanachama pia utajadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye
Halmashauri zao za sekta ya maji, barabara na majengo.
Mhandisi Kunyaranyara
alisema kuwa pia mkutano huo utajadili mfumo wa watumishi wa taaluma ya
Uhandisi wa serikali za Mitaa ili kuona kama lengo la kuwa na wahandisi wanne
kila Halmashauri limefikiwa katika Idara ya Uhandisi ikiwemo wasaidizi katika
Idara za maji, barabara na majengo.
Aidha mkutano huu
utawashirikisha pia wajumbe wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Bodi ya Usajili ya
Wakandarasi na Bodi ya Wasanifu na Wakadiriaji wa Majengo ili kuwezesha
kujadili na kusaidia miradi inayotekelezwa kwenye Halmashauri kutoharibika kwa
muda mfupi baada ya kukamilika kwake pamoja na kuangalia mafanikio ya miaka 8
toka kuanzishwa kwake rasmi mwaka 2007.
Rais, Kunyaranyara
alieleza kuwa katika mkutano huo wajumbe watapata fursa ya kujadili kwa kina na
kushauri juu ya utekelezaji wa miradi ya maji, majengo ikiwemo ujenzi wa Vyumba
vya maabara, utumiaji wa mitambo ya umeme na vifaa vya kudrufu, kusaidia
wanafunzi wa kike wa sekondari kusoma masomo ya Sayansi kusaidia vitabu.
Ameongeza kuwa mkutano huu
watautumia kutoa msaada wa madawati 100 kwa shule moja ya Msingi iliyopo katika
Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kutembelea ujenzi wa miradi ya barabara za mawe
za halmashauri ya Jiji la Mwanza na mgeni rasmi atakayefungua mkutano wetu wa
mwaka ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Faizal Issa,
Naye Makamu wa Rais wa
ALGETA, Mhandisi Gerald Matindi, alisema mkutano huo utahudhuliwa na Wahandisi
wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Wilaya, Sekretarieti za Mikoa na Wizara ya
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambapo pia utekelezaji wa
rasilimali watu na fedha zinavyofanikiwa.
Amesema kuwa mkutano huu utaishauri
serikali kuhusu taratibu za manunuzi ya umma ambao umekuwa na changamoto
zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuchelewa
kukamilika kwa wakati kutokana na sheria na taratibu za manunuzi ya umma kuwa
katika Idara nyingine badala ya kuwa Uhandisi
Kwa upande wake Katibu
Mkuu wa ALGETA, Mhandisi Lusekelo Mwakyami, alisema kuwa mkutano huo utatoa
mapendekezo kwa serikali ili kuanzisha mchakato wa ujenzi wa maabara za Kanda
za Uhandisi kama ilivyo kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) ili kuwezesha
kufanyia vipimo sampuli na malighafi za ujenzi wa miradi ili kuwa na ubora na
iweze kudumu kwa muda mrefu baada.
Ametoa wito kwa
wanachama wote kuhudhulia mkutano huo ambao umelenga kuboresha utoaji huduma na
utekelezaji bora utakaoendana na thamani ya fedha katika miradi hiyo kwenye
Halmashauri zao na kuhusisha wajumbe wa ERB na CRB kutawezesha kudhibiti kwa
wenye fedha kufanya ujenzi wa majengo kwa kufuata taratibu na sheria ili
kutoharibu sifa ya wahandisi.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment