Suala la kubaini kaya
maskini nchini linalotokana na mpango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF awamu ya tatu linapaswa kufanyika kwa umakini ili kuondoa migogoro na utata unaoweza kujitokeza katika jamii.
Hii itasaidia walengwa
waliokusudiwa kunufaika kutokana na ukweli kwamba zipo kaya nyingi nchini
ambazo ni maskini lakini zinazotarajiwa kunufaika na mpango huo ni zaidi ya
kaya miloni moja.
Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale Mkoani Geita Ibrahim Marwa akisisitiza jambo kwa wajumbe wakati wa kikao elekezi cha kubaini kaya maskini. |
Tatu Mwaruka Afisa wa kuboresha Maisha ya Jamii TASAF Makao makuu akielezea wajumbe wa wilaya ya Nyang'hwale Mkoani Geita namna walivyojipanga katika awamu hii. |
Mhandisi Barnabas Jachi Kamu meneja wa miradi ya Kutoa ajira makao makuu TASAF ambaye pia ni mtaalam wa mazingira |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang'hwale Fortunata Malya akisimama kuelezea furaha yake kupokea mpango huu wa TASAF 3 wa kunusuru kaya maskini katika wilaya hiyo. |
Baadhi ya wajumbe wa kikao elekezi cha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF 3 cha namna ya kubaini kaya maskini katika wilaya ya Nyang'hwale Mkoani Geita wakimsikiliza Mkuu wa wilaya hiyo Ibrahim Marwa hayupo pichani wakati akifungua kikao hicho
Mkuu wa wilaya ya
Nyang’hwale Mkoani Geita Ibrahim Marwa ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa
mpango wa TASAF awamu ya tatu wilayani huo.
Amesema ana amini kuwa viongozi
ambao wamepewa jukumu la kusimamia
katika kubaini kaya maskini watazingatia taratibu , kanuni na vigezo
ambavyo vimewekwa ili walengwa wanufaike.
Akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi mkuu wa TASAF Taifa Kaimu meneja miradi ya kutoa ajira ambaye pia
ni mtaalam wa mazingira kutoka makao makuu ya TAFAS mhandisi Barnabas Jachi anaelezea yaMNA YA kubaini kaya maskini ili ziweze kunufaika na
mpango huo.
Mratibu wa TASAF wilaya ya
Nang’hwale Nashon Magumba na baadhi ya wajumbe ambao wameshiriki katika uzinduzi huo ambao
umeambatana na mafunzo ya namna ya kuzitambua kaya maskini wanaelezea jinsi
ambavyo wameupokea mpango huo.
Mpango wa TASAF awamu ya tatu katika wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita utavinufaisha vijiji 40 kati ya 62 , kaya zaidi 2, 500 katika awamu hii.
Mwisho
No comments:
Post a Comment