Kufuatia kipigo cha mabao
sita kwa moja kutoka kwa timu ya soka ya Mwanza Queen katika masshindano ya
kombe la Taifa kwa wanawake timu ya soka ya wanawake ya Mkoa wa Mara imeweka
kambi kwa ajili ya kulipiza kisasa katika mchezo wa marudiano.
Timu hiyo ya wanawake ya
Mkoa wa Mara imeweka kambi jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
kulipa kisasi ili iweze kusonga mbele katika mashindano hayo.
Ni wachezaji wa timu ya soka ya wanawake ya Mkoa wa Mara Mara Queens wakiwa
wanajifua jijini Mwanza katika
mazoezi makali kwa ajili ya kujiandaa na
mchezo wa marudiano baina ya timu
ya soka ya wanawake ya Mkoa wa
Mwanza Mwanza Queens.
Star Tv
imeshuhudia wachezaji hao wakifanya mazoezi hayo na kuelezea matumani
yao katika mchezo wa marudiano Mkoani Mara huku wakilalamikia uongozi wa Mkoa
wa Mara kwa kushindwa kuwasaidia vifaa vya michezo.
Katibu wa
Mara Queens Sure Mugeta amesema wameweka kambi
jijini Mwanza kutokana na
kudhaminiwana na mdau wa michezo ambaye ni m kurugenzi wa
kituo cha michezo cha Alliance James Bwire na kutoa wito kwa wadau wengine wa
Mkao wa Mara kuiga mfano huo kwa kutoa msaada wa hali na mali ili
waweze kufanya vizuri zaidi.
Kocha Mkuu
wa timu hiyo Msakato Magai amesema anauhakika wakufanya vizuri katika mchezo wa
marudiano kutokana na mazoezi ambayio wameyafanya na wachezaji wake wote wako
vizuri.
Katika
mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa kuwania kombe la Taifa la wanwake baina ya Mara Queens na Mwanza Queens timu hiyo ilichpwa mabao sita kwa moja na
mchezo wa marudiano baina ya timu
hizo unapigwa katika uwanja wa Karume
mjini Musoma January 13 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment