Ongezeko la uhaba wa chakula na umaskini kwa baadhi ya kaya za mikoa ya kanda ya ziwa unatokana na wakulima kutofikiwa na elimu ya kilimo kinachostahimili ukame na chenye tija.
Wakulima wametakiwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa kilimo kwa kujikita katika kulima zao la Mtama badala ya zao la mahindi linalotegemewa zaidi kwa chakula ili kukabiliana na balaa la njaa kwa baadhi ya kaya za mikoa ya kanda ya ziwa.
Mkoa wa Mwanza ni moja ya mikoa ambayo inapata mvua chini ya wastani milimita 750 kwa Mwaka ambayo inafaa kwa kilimo cha mahindi hali inayosababisha uhaba wa chakula wa kaya kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
No comments:
Post a Comment