Mbele ni Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi na mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Mwanza MZFA Jackson Songora facebook akiwa na ujumbe kamili wakielekea kwenye viwanja vya michezo vya kituo cha michezo cha Alliance wakati wa ziara yake ya kukagua viwanja hivyo. |
Shirikisho la soka nchini
TFF limeridhishwa na maandalizi ya viwanja vitakavyotumika katika mashindano ya
Taifa ya soka la vijana walio chini ya umri wa miaka 13.
Rais wa Shirikisho hilo
Jamal Malinzi ametoa kauli hiyo jijini Mwanza baada ya kukagua viwanja vya michezo vya
Alliance ambavyo vitatumika katika mashindano hayo ambayo yamepangwa kufanyika
jijini Mwanza Aprili Mosi mwaka huu.
Malinzi
amesema kuwa mashindano ya soka ya Taifa ya vijana yana umuhimu wake hivyo ni vema wadau wa soka kwa ujumla wakaunga
mkono jitihada zinazofanywa na kituo cha
michezo cha Alliance.
Katika hatua
nyingine Rais huyo ameonywa viongozi wa vyama vya soka vya mikoa kutoanda a
vijana wenye umri mkubwa tofauti na wale waliochini ya umri wa mika 13 katika
mashindano hayo.
Amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuunda timu ya Taifa ya vijana ambao wataweka kambi ya mika mne kabla ya kuanza kwa mashindano ya AFCON
mwaka 2019
Mkurugenzi
wa kituo cha michezo cha Alliance James
Bwire amesema kufuatia ziara ya Rais wa
Shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi katika kituo hicho wataendelea kufanya
marekebisho ya liyobaki katika viwanja hivyo.
Kutokana
na umuhimu huo mkurugenzi wa Alliance amemuomba Rais wa TFF kumuagiza
mtaalam wa kutengeneza viwanja vya michezo kuja jijini Mwanza kwa ajili
ya kusaidia marekebisho ya viwanja hivyo kabla ya kuanza kwa mashindano
ya vijana waliochini ya umri wa miaka 13.
Malengo ya
mashindano ya soka kwa vijana waliochini ya umri wa miaka 13 ni kuunda timu ya
Taifa ya vijana ambayo itaweka kambi ya mika mine kabla ya kushiriki mashindano
ya AFCON mwaka 2019 ambapo Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.
Uwanja huu pia unaandaliwa kwa ajili ya kutumika kwa mashindano ya Taifa ya soka ya vijana ambayo yatashirikisha mikoa ya Tanzania |
Rais wa TFF Jamal Malinzi akiwa na ujumbe wake wakati wa ziara ya kukagua maendelea ya maandalizi ya viwanja katika kituo cha michezo cha Alliance jijini Mwanza |
Add caption |
Kulia ni Mkurugenzi wa kituo cha michezo cha Alliance cha jijini Mwanza James Bwire akiowaelekeza wajumbe wa walioambatana na Rais wa TFF Jamal malinzi wakati wa ziara yake katika kituo hicho. |
No comments:
Post a Comment