WILSON KOLINA ELISHA

WILSON KOLINA ELISHA

BLOG HII NI MUHIMU KWA JAMII KUTOKANA NA KUJIKITA KATIKA KUANDIKA HABARI TOFAUTI ZA UHAKIKA NA ZILIZOFANYIWA UCHAMBUZI WA KINA...........

Thursday, January 8, 2015

RC MWANZA AZINDUA MALANDO CUP HUNG'HUMALWA KWIMBA


MKUU wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mlongo amezindua mashindano ya soka ya Malando Cup katika kata ya Hung'humalwa wilayani Kwimba.

Akizungumza  baada ya kuzindua mashindano hayo amesema anatambua kuwa lipo tatizo la ukosefu wa viwanja vya michezo na vifaaa vya michezo katika maeneo mbalimbali Mkoani Mwanza jambo ambalo  ni moja ya sababu zinazochangia kazi ya kuvumbua, kukuza na kuendeleza vipaji vya wanamichezo kutofanyika kwa ufanisi.

Kutokana na hali hiyo wadau wanapaswa kuona umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika kukabiliana na tatizo hilo ambalo linawafanya vijana wengi washindwe kuonyesha vipaji vyao huku Taifa likikosa wanamichezo wanaoweza kuiweka nchi katika ramani ya dunia katika michezo

   Amesema michezo haijengi  uadui,  bali hujenga undugu, urafiki na huimalisha mahusiano,  baina ya wanamichezo na viongozi,  hivyo ni vema ikatumika kwa  malengo ambayo yamekusudiwa 

Aidha Mkuu huyo analiona suala la zawadi kuwa nila muhimu  na kuahidi kuwazawadia washindi wa tatu wa juu katika timu zinazoshiriki mashindano hayo ambapo bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha shilingi Laki mbili huku mshindi wa pili akijipati shilingi Laki moja na nusu mshindi watatu ataambulia shilingi Laki moja.


  Amesema michezo haijengi  uadui,  bali hujenga undugu, urafiki na huimalisha mahusiano,  baina ya wanamichezo na viongozi,  hivyo ni vema ikatumika kwa  malengo ambayo yamekusudiwa 


Mdhamini  wa mashindano hayo Shija Malando anasema ameamua kuanzisha mashindano hayo ambayo anaamini yatakuwa chachu kwa vijana na wakazi wa kata hiyo.

Ameongeza kuwa baada ya kumalizika kwa mashindano hayo anatarajia kuanzisha mashindano mengine aqmbayo atawashirikisha wazee katika mchezo wa bao, wakimbiza baiskeli, mchezo wa wavu na wanawake kwa uapnde wa soka na mchezo wa Netiboli.

"Hiyo ni mikakati yangu ya badaye ambayo nina imani wilaya nzima ya Kwimba itaiga mfano ambao nimeuanzisha kwa kufufua michezo ya aina tofauti," amesema Malando
            
Mashindano hayo yenye lengo la kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 yanazishirikisha  timu nane za soka ambazo ziko  kata ya Hung’humalwa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.



 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mlongo akikagua timu za soka wakati wa ufunguzi wa Malando Cup 2014/ 2015


Mkuu wa Mkoa akisalimia na baadhi ya wachezaji wa timu zinazoshiriki Malando Cup huku nyuma ya mkuu wa Mkoa akiwa ni mdhamini mkuu wa mashindano hayo Shija Malando ambaye ni Diwani wa kata ya Hung'humalwa wilayani Kwimba

Mkuu wa wilaya ya Kwimba Seleman Mzee akionyesha baadhi ya vipaji vya wanamichezo katika mchezo wa ufunguzi wa kuwania Malando Cup 2014/2015

Sehemu ya jukwaa kuu wakiwa wanatazama kwa umakini jinsi mchezo wa ufunguzi unavyoendelea katika uwanja wa Mnadani kata ya Hung'humalwa.





Kulia ni mdhamini wa mashindano hayo Shija Malando  alipokuwa anatoausia kwa baadhi ya wanamichezo wa timu zinazoshiriki mashindano hayo



Sehemu ya mashabiki wa sok awaliofurika katika uwanja wa Mnadani kushuhudia mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Malando Cup
.

No comments:

Post a Comment