Mkurugenzi wa timu ya soka ya Alliance Academy James Bwire akishiriki mazoezi ya GYM pamoja na wachezaji wa timu yake |
TIMU ya soka ya Alliance Academy ya jijini Mwanza imepania kutwaa ubingwa wa Mkoa wa Mwanza katika ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa hatua ya fainali ambayo inatarajiwa kuanza Disemba 31, 2014 .
Hatua ya fainali inazishirikisha timu 12 zilizofuzu kutoka hatua ya makundi ambayo ilikuwa na timu 29 katika ligi hiyo ya mkoa wa Mwanza.
Mkurugenzi wa timu hiyo James Bwire amesema kuwa wamejipanga vema kukabiliana na timu zinazoshiriki hatua hiyo na hii ni kutokana na kufanya mazoezi yenye lengo la kufanya vizuri zaidi.
Alliance inanza kusaka ubingwa wa Mkoa wa Mwanza kwa kumenyana na timu ya soka ya Sengerema Stars katika uwanja wa Mnadani mjini Sengerema katika mechi ya ufungunzi.
Mkurugenzi huyo ameyataja baadhi ya mazoezi ambayo timu yake imeyafanya kuwa ni pamoja na mazoezi ya GYM huku anye akishiriki katika GYM ya Family Fitness Fortest ya jijini Mwanza ambayo anaamini yatakuwa muarobaini katika kusaka ubingwa wa mkoa.
Amesema kwa kawaida mazoezi ya GYM yamekuwa yakitumiwa na klabu kubwa duniani ambapo hapa nchini klabu za Simba na Yanga ndizo zenye utaratibu wa aina hiyo.
Ametoa wito kwa wadau na wapenzi wa soka wa timu hiyo kuiunga kwa kuishangilia kila inapocheza michezo yake katika hatua hiyo ya fainali ambayo anaamini ni ngumu kwani kila timu iliyofuzu katika hatua hiyo ni nzuri na imejiandaa .
Kocha mkuu w atimu hiyo Furgence Novatus amesema katika kikosi chake hakuna majeruhi hata mmoja wote wako katika hali nzuri na mategemeo yake ni kuendeleza ubabe kwa timu ya Sengerema Stars na hii ni kutokana na timu hiyo kupata ushindi wa mabao 2- 0 dhidi ya timu hiyoi katika hatua ya makundi katika kituo cha Sengerema.
Katikati ni mkurugenzi wa Blog hii akiwa na makocha wa timu ya Alliance Sports |
kATIKATI NI Mmoja wa makocha wa timu ya Alliance Kessy Mziray akiwa na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo baada ya vkumaliza mazoezi ya GYM |
No comments:
Post a Comment