Baadhi ya miundo mbinu ya maji katika wilayani Nyang'hwale Mkoani Geita ikiwa imeharibika |
Mwenye shati nyeusi ni mkurugenzi wa Blog hii akifanya mahojiano na mkazi wa Kharumwa wilayani Nyang'hwale Mkoani Geita Bw. Henry Wilson juu ya hali ya upatikanaji wa maji. |
Upo usemi usemao kuwa kazi ni kazi bora mkono uende kinywani ilimradi kazi hiyo iwe halali. Huo ni usemi ambao watu wengi wanashindwa kuutafisri vizuri na hivyo kuendelea kulalamikaii.
Hiyo ni kauli ya Henry Wilson mkazi wa Kharumwa akielezea jinsi anavyonufaika na shughuli ya kuchota maji .
Henry alisema kuwa kazi ya kuchota maji anaifanya kila siku na ameifanya zaidi ya miaka mitano ambapo ndoo moja ya lita ishirini anauza shilingi mia mbili hamsini wakati wa masika huku wakati wa kiangazi anauza ndoo moja kwa kiasi cha shilingi 1000.
Amebainisha kuwa kwa siku anauwezo wa kuuza zaidi ya ndoo 70 kwa wateja wake ambao
Amesema kutokana na kazi hiyo ameweza kujjenga nyumba na anaitunza familia yake vizuri na ameahidi kuendelea kufanya kazi hiyo kwani ina manufaa zaidi.
Hata hivyo amelalimikia kitendo ambacho watu wasiojulikana waliweza kuharibu miundombinu ya maji na kutoa wito kwa ngazi husika kufanya kila jitihada kuwabaini wahusika ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Kutokana na vijana wengi kukaa kijiweni bila kufanya kazi ametoa wito kuachana na tabia hiyo na badala yake wawajibike ili wajikwamue na umaskini na wasibague kazi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment