WILSON KOLINA ELISHA

WILSON KOLINA ELISHA

BLOG HII NI MUHIMU KWA JAMII KUTOKANA NA KUJIKITA KATIKA KUANDIKA HABARI TOFAUTI ZA UHAKIKA NA ZILIZOFANYIWA UCHAMBUZI WA KINA...........

Wednesday, February 4, 2015

GERFA YATANGAZA TAREHE YA KUANZA HATUA YA NANE BORA


CHAMA cha soka Mkoani Geita GERFA kimetangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa hatua ya Nane bora ya ligi soka daraja la tatu katika harakati za kusaka ubingwa wa Mkoa huo.

Akizungumza na blog hii wilayani Nyang'hwale  Mkoani Geita katibu mkuu wa chama hicho Robert Machimu amesema kuwa hatua hii inaanza kufuatia kumalizika kwa hatua ya kwanza ambayo ilikuwa ikizishirkisha timu 16.

Machimu amesema kuwa hatua ya Nane bora imepangwa kuanza Februari Nane mwaka huu kwa kuzishiriksha timu kutoka katika wilaya nne kati ya tano zinazounda mkoa huo  ambazo zitachuana katika viwanja mbalimbali.

Machumu amezitaja timu ambazo zimefuzu kucheza katika hatua hiyo kuwa ni Ukillinya Fc  Chato Stars,Kigo Fc,  Vijana Fc Chato,  Iponya Fc,  black Mamba , Ibamba Fc na  Nyaluminiamu FC.

Ameongeza kuwa hatua ya awali ilikuwa na ushindani mkubwa hivyo ana matumaini kuwa hata hatua hii ya Nane bora itakuwa na ushindani zaidi.

Machimu amesema timu zilizofuzu katika hatua hiyo zimenufaika na udhamini wa Taasisi ya Mtalitinya Foundation ya Mkoani Geita kwa kupewa vifaa vya michezo ikiwemo jezi, viatu  na mipira ambapo pia unahusisha na utoaji wa semina kwa wacheazi na viongozi juu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Amefafanua kuwa kuwepo kwa udhamini huo ambao niwa zaidi ya shilingi milioni Nane ni jambo ambalo linasaidia timu shiriki kuwa na uhakika wa kuongeza kasi ya ushindani katika ligi hiyo kwa timu zinazoshiriki.

Mashabiki wa soka wametakiwa kuhudhuria michezo ya hatua ya Nane bora ili kuleta hamasa kwa wachezaji wao ambao watakuwa wanatafuta nafasi ya kutwaa ubingwa wa Mkoa wa Geita.

Kutokana na udhamini wa Taasisi ya Jacob Mtalitinya Foundation ametoa wito kwa Taasisi nyingine kujitokeza kudhamini ligi hiyo kwani bado wanahita ili kuweza kuendeleza soka Mkoani humo.

Mwisho****************************




No comments:

Post a Comment