Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Kabole Kahungwa amesema kuwa wametoa msada huo ikiwa ni sehemu ya kuthamini na kutambua umuhimu wa michezo hasa kwa wachezaji wa zamani ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuimarish aafya zao sanjari na kujenga mahusiano baina ya wanamichezo.
Kahungwa amesema kuwa wataendelea na utaratibu wa kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu nyingine za Veteran ili iwe moja ya hamasa kwa timu hizo kupenda kushiriki michezo.
Amebainisha kuwa anatambua zipo chanagmoto nyingi katika tasinia ya michezo hususani vifaa hivyo kutolewa kwa vifaa hivyo ana amini vitasaidia kupunguza tatizo hilo nakuahidi kuendelea kushirikiana na wadau katika kuinua vipaji.
Kwa upande wake mweneykiti wa timu ya Rocky City Veteran yeney maskani yake Mabatini jijini Mwanza Munga Lupindo ambaye pia ni katibu wa Chama cha soka wilaya ya Nyamagana NDFA ameshukuru kampuni ya The Bright Platform Co. Ltd kwa msaada huo na kusema msaada huo umetolewa muda mwafaka ambapo walikuwa wakikabiliwa na upungufu wa vifaa vya michezo.
Munga ametoa wito kwa makampuni mengine watu binafsi na taasisi mbalimbali kujitokeza kusaidia timu zinazoundwa na wachezaji wa zamani maarufu Veteran ili waendelea kujenga afya zao ana kuimarisha mahusiano.
Vifaa ambavyo vimetolewa ni pamoja na mpira mmoja na jezi seti moja
Mwenye tishet ya Punda milia ni mkurugenzi wa The Bright Platform Co. Ltd akikabidhi vifaa vya michezo kwa viongozi wa timu ya soka ya Rocky City Veteran |
No comments:
Post a Comment