MKATABA SOKA GEITA
Na Wilson Elisha
Geita
03/10/2013
Chama cha soka Mkoa wa Geita GERFA kimetiliana saini mkataba
wa kudhamini ligi ya mkoa huo hatua ya Nane bora baina ya Taasisi ya Mtalitinya Foundation kwa kipindi cha misimu miwili kuanzia mwaka 2013/2014
hadi 1015 wenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 16.
Mkataba huo utajikita katika kuvumbua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana katika michezo sanjari na masuala ya
Maendeleo, uchumi Afya na Ukimwi.
Hafla fupi ya kutiliana saini mkataba wa udhamini wa ligi ya Mkoa wa Geita ambayo
imehudhuriwa na wadau mbalimbalu kutoka mkoani humo imefanyika katika Ukumbi wa Nkola ulioko Mjini Geita.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa
Geita Leonard Paulo amesema udhamini huo
umetolewa na mdau mwelevu ambaye anathamini na kutambua umuhimu wa maendeleo hivyo ni
vema wadau wengine wakaunga mkono jitihada hizo ili kuweza kupata manufaa zaidi
na kufikia malengo ya kundeleza michezo.
Kwa upande wake mdhamini mkuu wa ligi
hiyo ya Mkoa wa Geita kupitia Taasisi yake ya Mtalitinya Foundation , Jacob Mtalitinya amewatahadharisha viongozi wa vyama
vya michezo kuachana na tabia ya kujikita katika migogoro na
kuleta ugomvi badala ya kujikita katika mipango ya kuwaletea maendeleo
wanamichezo.
Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoa wa Geita GERFA, Salum Kulunge amesema anaamini
kuwa kusainiwa kwa makataba huo ni historia katika mkoa huo ikiwa ni mwaka mmoja tangu waingie madarakani mOktoba mwaka jana 2012.
Amebainisha kuwa mkataba huo ni mkubwa sana hivyo chama chake kinampongeza mdhamini mkuu wa ligi ya Mkoa wa Geita na kuwaomba wadau wauunge mkono na si kuubeza kwani zipo ligi nyingi katika mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar hawajapata wadhaminnji wa ligi zao.
Mratibu wa
Taasisi ya Vijana na maendeleo ya Mtalitinya Foundation ambayo imedhamini ligi hiyo David Azaria amesema kuwa washindi watazawadiwa zawadi mbalimbali ikiwemo kombe na fedha taslimu Az
VOX:2
1.Salum Kulunge –
M/Kiti GEDFA
2.David Azaria –
Mratibu wa Mtalitinya Foundation
Mkataba huo
utazihusisha jumla ya timu Nane ambazo zitatinga katika hatua ya robo fainali
kwa kipindi cha misimu miwili huku
bingwa akizawadiwa kombe na kitita cha shilingi Milioni moja, mshindi wa pili
shilingi Laki tano na mshindi wa tatu shilingi laki mbili na nusu.
Mwisho
SIGN OFF
No comments:
Post a Comment