WACHUNGAJI
Na Wilson Elisha
Mwanza
Wachungaji wa madhehebu ya
dini nchini wameaswa kuyatumia
maandiko matakatifu ya Mungu kwa usahihi kuwafundisha wanadamu ili waweze kutenda mema na kuepusha maovu yanayochangia ongezeko la watu wenye dhambi duniani.
Akihubiri
katika mahafali ya sita ya chuo kikuu cha Mount Meru cha kanisa la Baptist tawi
Mwanza, mchungaji Joseph Kahindi amesema
kuwa wachungaji bado wanayo nafasi kubwa ya kubadili maisha ya wanadamu kuacha maovu.
Amesema kuwa hatua hii itasaidai wanadamu kuepukana na dhambi ambazo mwisho wake ni mauti jambo ambalo ni hatari miongoni mwa jamii.
Mchungaji
Kahindi ambaye pia ni mkuu wa
kitengo cha Theolojia katika chuo kikuu cha Mount Meru amesema ni vema wachungaji wakazingatia maadili ya
kiuchungaji katika kuwafundisha wanadamu ambao wamelemewa na mzigo wa dhambi.
Amesema hivi sasa ulimwengu umekubikwa na majanga mbalimbali ambayo yanachangia mmomonyoko wa maadili kwa wanadamu kuwa mkubwa na kujiingiza katika vitendo vya kumuasi Mungu.
Amefafanua kuwa kutokana na kuhitimu wachungaji ni muhimu wakitumia elimu waliyoipata katika kuwakomboa wanadamu ili wasiendelee kuangamia na dhambi.
Awali
mwangalizi wa makanisa ya Baptist kanda ya ziwa mchungaji Boniphace Mponeja
alielezea juu ya mchango unaotolewa na wachungaji katika jamii.
Alisema kuwa wachungaji wanapaswaa kuwa mstari wa mbele katika kufanya kazi kwa umakini kwani kazi inamjengea heshima mwanadamu sanjari na kujitafutia riziki halali.
Mkurugenzi
mkazi nchini kutoka Chuo kikuu cha Mount Meru Nancy Giddens amesema jukumu walilonalo
ni kutoa elimu kwa wachungaji ili waweze kujikita katika kuwafundisha wanadamu.
Mkurugenzi mkazi huyo alisema kuwa licha ya changamotoi zilizopo katika kuwafundisha wachungaji na wake wa wachungaji lakini bado uongozi wa Chuo kikuu cha Mount Meru unaendelea kujitahidi ili kuepukana na chnagmoto hizo.
Katika
mahafali hayo ya sita ambayo yamefanyika katika kanisa la Baptist jijini Mwanza
wachungaji 21 wametunukiwa vyeti bada ya kuhitimu na kufuzu masomo ya THEOLOJIA,
huku wake wa chungaji 16 wakitunukiwa
vyeti vya biblia na huduma ya kikristo.
No comments:
Post a Comment