WILSON KOLINA ELISHA

WILSON KOLINA ELISHA

BLOG HII NI MUHIMU KWA JAMII KUTOKANA NA KUJIKITA KATIKA KUANDIKA HABARI TOFAUTI ZA UHAKIKA NA ZILIZOFANYIWA UCHAMBUZI WA KINA...........

Tuesday, March 25, 2014

MAC Adverts co mwanza yaandaa tamasha la kifamilia

MAC Adverts co Mwanza imeanda tamasha kubwa la kifamilia ambalo limepangwa kufanyika katika viwanja vya YATCH CLUB CAPRI POINT jijini Mwanza Jumamosi ya Machi 29 mwaka huu.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Hally Mbilinyi ameieleza blog hii kuwa maandalizi yote yamekwisha kamilika na litaanza kwa muda uliopangwa ambao ni saa sita mchana.

Ametoa wito kwa wanafamilia kutoka mkoa wa mwanza na mikoa ya kanda ya ziwa na Tanznaia kwa ujumla kuhudhuria tamasha hilo ambalo anaamini litakuwa lenye mafanikio makubwa miongoni mwa washiriki.

Amefafanua kuwa tamasha hilo litasheheni michezo mbalimbali pamoja na burudani ambapo  kutakuwa na zawadi kwa washindi wa michezo mbalimbali.

Ameitaja baadhi ya michezo hiyo kuwa ni pamoja na pool table , mpira wa meza, pia watoto watapata fursa ya kushiriki michezo mbalimbali na washiriki wataweza kuona michezo yote ya siku hiyo  itakayochezwa katika ligi ya Uingereza, Hispania na Ujerumani kupitia Channel ya DSTV .

Akizungumzia suala la ulinzi na usalama kwa watakaoshiriki tamasha hilo mkurugenzi matendaji huyo amesema kuwa utaimarishwa hivyo amewaondolea wasiwasi wale wote watakapata nafasi ya kushiriki tamasha hilo.

Ratiba yavtamasha hilo inaonyesha kuwa michezo  inatarajiwa kuaanza saa sita mchana hadi saa tatu usniku

Kiingilio katika tamasha hilo ni shiulingi elfu tano kwa watu wakubwa na watoto itakuwa ni shilingi elfu mbili.

Mwisho
 



No comments:

Post a Comment