BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WAKIWA KATIKA ENEO LA TUKIO |
HII NI SEHEMU YA MADUKA YA WAFANYABIASHARA YAKIWA YAMEFUNGWA |
BAADHI YA WANANCHI WAKIANGALIA VURUGU ZILIZOKUWA ZIKIENDELEA |
BAADHI YA VIBANDA VYA WAMACHINGA VILIVYOBOMOLEWA
BAADHI YA MABAKI YALIYOBOMOLEWA NA KUCHOMWA MOTO NA WAMACHINGA NA BAADAYE YA KUZIMWA NA JESHI LA POLISI
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA CHRISTOPHER FUIME
HIZI NI PICHA MBALIMBALI ZINAZOONYESHA TASWIRA YA JIJI LA MWANZA ILIVYOKUWA KUTOKANA NA VURUGU ZILIYOTOKEA BAINA YA ASKARI POLISI NA MACHINGA WA JIJINI HUMO.
Jiji la Mwanza liligeuka kuwa uwanja wa mapambano kutokana na vurugu baina ya wamachinga na jeshi la polisi baada ya wamachinga wanaofanya biashara katika eneo la TEMBO Maarufu Makoroboi
kukuta vibanda vyao vikiwa vimebomolewa na mgambo wa jiji kwa kushirikiana na polisi.
wakizungumza baada ya tukio hilo baadhi ya wamachinga wamelalamikia kitendo hicho na kusema hakikuwa cha kiungwana licha ya matangazo kutolewa mara kadhaa na mamlaka ya jiji hilo ya kuwataka kuondoka katika eneo hilo.
Aidha wananchi wakawaida pia wamelaumu na kusema kwamba ingetumika kabla ya maamuzi hayo yaliyotekelezwa na jeshi la polisi
akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mwanza mrakibu mwandamizi wa polisi Christopher Fuime amesema kuwa hawatavumilia kuona sheria zikikiukwa huku jeshi hivyo ni vyema watu wakazingatia taratibu zilizowekwa na kutii sheria bila shuruti."ZOEZI HILI NI ENDELEVU".
No comments:
Post a Comment