Na Wilson Elisha
Mwanza
Baadhi ya wakzi wa jiji la Mwanza waliokuwa katika mitaa ya sokoni na Lumumba karibu na msikiti wa Ijumaa jijini humo walijikuta wakiwa katika wakati mgumu kufuatia mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mitaa hiyo kufurika maji.
Licha ya barabara za mitaa hiyo kujengwa kwa kiwango cha rami lakini imekuwa kero kwa wakazi hao hasa pale mvua zinaponyesha kwani mitaro haipitishi maji.
Blog hii ilishuhudia barabara za mitaa hiyo zikiwa zimefurika maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha takribani masaa mawili na kusababisha usumbufu kwa wakazi waliokuwa katikati ya jiji la Mwanza.
Baadhi ya wakazi wa jijin la Mwanza wakizungunmza na blog hii walisema ni aibu kwa jiji la Mwanza ambal.o linasifiwa kwa usafi kwa kushika nafasi ya kwanza mingoni mwa majji hapa nchini kwa kipindi za zaidi ya miaka mitano mfululizo kuona mitaro ikishindwa kupitisha maji.
Ashura Khamis mkazi wa Pasiansi jijini hapa alisema kuwa ni vema hatua za maksudi zikachukuliwa kurekebisha mitaro katika mitaa hiyo ili kuondoa aibu ya jiji la Mwanza hasa pale mvua zinaponyesha inakuwa ni kero
Aliongeza wakazi wa jiji la Mwanza wanapata usumbufu mkubwa hasa pale wanapotaka kwenda kupanda daladala za Mwaloni, Kirumba, Kitangiri, Bwiri, Ghana, Kona ya Bwiru, Nyamanoro, Pasinasi, Ilemela mahakamani na Airpot.
"Ni vema viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia jiji la Mwanza wakafanya kila jitihada za kuondoa kero hiyo inayolitia aibu jiji la Mwanza wakati wa masika,"alisema
Kwa upande wake Peter Amada mkazi wa Bwiru alisema kuwa wanapata adha wanapotaka kwenda kupanda daladala mvua kuybwa inapokuwa imenyesha kwani barabara zinajaa maji ambapo kituo kiko mtaa wa sokoni.
Wanaiomba mamlaka inayohusika kunusuru hali hiyo ambayo wamekuwawakiipata kwa muda mrefu
jambo wanashindwa kuelew ni kwa nini lisitafutiwe ufumbuzi wa kudumu.
Kila mvua kubwa zinaponyesha baadhi ya maeneo ya jiji la Mwanza yamekuwa yakijaa maji na kuleta usumbufu kwa wananchi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment