Na Wilson Elisha
Sengerema
Halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imepitisha zaidi ya shilingi Bilioni 63.2 katika mwaka wa fedha 2014/2015 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Kiasi hicho cha fedha kimepitishwa katika kikao cha Baraza la madiwani kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo chini ya mweneyhkiti wake Mheshimiwa Mathew Lubongeja.
Katika kikao hicho ambacho kimewashirikisha wataalam wa idara mbalimbali mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Danstan Mallya amesema kupitishwa kwa bajeti hiyo kutasaidia kuendeleza miradi katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema itaendelea na jukumu la utoaji wa huduma za kijamii na kiuchumi kwa kuzingatia dira ya Taifa 2025 na malengo ya Melenia na Mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini Tanzania MKUKUTA.
Aidha Halmashauri hiyo itaimarisha mfumo wa sheria na utawala bora kuanzia ngazi ya vijiji sanjari na kuboresha masuala ya mtambuka kama vile jinsia , mazingira rushwa na ukimwi.
Aliongeza kuwa ushirikishwaji wa jamii katika kupanga, kutekeleza na kutathimini miradi yao ya maendeleo na uboreshaji wa mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri, pia ni mkakati mwingine wa kuiweka jamii kutambua umuhimu wa ushirikishwaji.
Akizungumza katika kikao hicho chas Baraza la madiwani Mkuu wa wilaya ya Sengerema Kalen Yunus amewasisitiza waheshimiwa madiwani kusimamia miradi yote iliyopitishwa ili kuleta tija katika jamii na kujikwamua na umaskini.
Alisema kuwa ni vema suala la ushirikishwaji wa jamiiiwapewa kipaumbele zaidi ili jamii ione umuhimu wa kuwepo miradi mbalimbali katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine mkuu huyo aliwaagiza wazazi na walezi kuhakikisha wanafunzi wote waliopata nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza wanaenda shule vinginevyo hatu akali za kisheria zitachukuliwa kwa wale watako kaidi agizo hilo.
Akifunga kikao cha Baraza la madiwani Mweneykiti wa Halmashauri hiyo Mheshimiwa Mathew Lubongeja alisema kuwa maagizo yaliyotolewa na mkuu wa wilaya hiyo watayatekeleza ili kuwaletea maendeleo wananchi wao.
Aidha alisema kuwa bajeti hiyo ni nzuri na imelenga kuwaletea maendeleo wananchi hivyo watashirikiana na wananchi sanjari anj wataalam wa idara mbalimbali katika kuona malengo yaliyowekwa yanafikiwa.
mwisho
No comments:
Post a Comment