WILSON ELISHA
MWANZA
Zaidi ya
shilingi Bilioni 18 zinatarajia kutumiwa
na Serikali za Tanzania na Canada katika kutekeleza mradi wa miaka mitatu na nusu wa Wazazi na Mwana
unaotekelezwa katika wilaya tano za
mikoa ya Mwanza na Rukwa.
Meneja wa mradi huo Dokta Safila Telatela alisema hayo baada ya kukabidhi simu za mkononi kwa mkuu wa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza Amina Masenza katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa manispaa ya Ilemela
Alibainisha kuwa mradi huo
unatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya watu milioni moja wakiwemo wanawake zaidi ya
laki tatu wenye umri wa kujifungua watoto, wanaume themenini elfu, watoto zaidi ya laki tatu na kuwajengea uwezo
wafanyakazi zaidi ya elfu moja, sanjari na wanajamii wapatao laki tano wa kujitolea katika vijiji 516.
Aidha meneja huyo alisema kuwa mradi unalenga kupunguza vifo
vya akinamama wajawazito, watoto wachanga na walio chini ya miaka mitano ambavyo vimekuwa vikitokea katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya mradi.
Alifafanua kuwa mradi huo unatekelezwa katika wilaya za Ilemela na Sengerema mkoani Mwanza, na wilaya za Nkasi, Sumbawanga vijijini na Kalambo mkoani Rukwa
utahakikisha unasaidia kuwasomesha madaktari na wauguzi watakaofanya kazi
katika vituo vya afya vitakavyotoa huduma ya upasuaji.
Alisema kuwa hivi sasa ujenzi wa vyumba vya upasuaji katika vituo vya afya vya mwangika na Sangabuye unaendelea na kwamba utakapo kamilika vitatolewa vifaa vya kiusasa kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa watakaopatiwa huduma ya uapasuaji.
Kwa upande wake Mkuu wa
wilaya ya Ilemela Amina Masenza mkoawa Mwanza Amina Masenza alisema kutolewa kwa simu hizo kutaboresha
rufaa za wagonjwa na kusaidia katika mawasiliano ya haraka pale ambapo ushauri
wa haraka unatakiwa ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
"Ninaamini simu zilizotolewa zitafanya kazi iliyokusudiwa ili malengo yaweze kutimia hususani kuoka maisha ya mama wajawazito, watoto wachanga na watoto chini ya miaka mitano,"alisema mkuu wa wilaya
"Sitegemei, sitarajii mtumishi yeyote aondoke na simu halafu aliyepozamu ahangaike kupata mawasiliano ya haraka kwa ajili ya wagonjwa watakaokuwepo katika vituo vya kutolea huduma," aliongeza mkuu huyo
Alibainisha kuwa mradi unafanya kazi katika vituo vya kutolea huduma vipatavyo 74 katika wilaya za Sengerema na Ilemela ambapo wilaya ya Ilemela inavituo 15 wakati wilaya ya Sengerema ina vituo 59.
Katika mradi huo tayari vituo vya afya vya Mwangika wilayani Sengerema na Sangabuye wilayani Ilemela vimekwisha patiwa magari ya kubebea wagonjwa.
Mradi huu unafadhiliwa na serikali ya CANADA kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na unatekelezwa na mashirika matatu yasiyo ya kiserikali ambayo ni Plan International, Africare na Jhpiego na unatarajia kufikia tamati Aprili mwaka 2015.
Mwisho
No comments:
Post a Comment