USHIRIKISHWAJI wa jamii na wadau mbalimbali katika mpango wa kunusuru kaya maskini nchini ni moja kati ya misingi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika kuhakikisha walengwa wananufaika na mpango huo.
Kauli hiyo imetolewa na Kaaimu Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa TASAF Chrisopher Sanga kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo Laudslaus Mwamanga wakati wa ufunguzi wakikao kazi kwa waratibu wahasibu wa mpango maafisa ufuatiliaji nawaandishi w ahabari kutoka mikoa ya Kagera, Shinyanga na Geita.
Baadhi ya waandishi wa habari ambao wameshiriki kikao kazi katika harakati za kunusru kaya maskini |
Baadhi ya waratibu wahasibu na maofisa ufuatiliaji wa mpango wa TASAF wakisikiliza mada katika kikao kazi pamoja na waandishi wa habari |
Ameongeza kuwa mafanikio ambayo yamekwisha patikana katika awamu hii ya tatu yametokana na ukweli kwamba ni ushirikiano uliopo baina ya watendaji na wanahabari katika utoaji wa habari zinazohusu nfuko huo kwa
Pamoja na mafanikio hayo bado kuna changamoto zilizopo kuhakikisha kaya masikini zinajikwamua hivyo kunahitajika maboresho zaidi.
Amebainisha kuwa TASAF ni chombo cha serikali kama mojawapo ya jitihada za kupunguza umaskini kwa kushirikiana na vyombo vingine vilivyopo.
Zuhura Mdungi Mkuu wa Kitengo cha Habari TASAF akitoa ufafanuzi wa jambo furani kwa washiriki wa kikao kazi |
Katika kikao hicho mada mbalimbali zimeweza kuwasilishwa ikiwemo uhaulisaji fedha na kimewashirikisha waratibu , wahasibu wa mpango maafisa ufuatiliaji na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Shinyanga, Geita na Kagera.
No comments:
Post a Comment