WILSON KOLINA ELISHA

WILSON KOLINA ELISHA

BLOG HII NI MUHIMU KWA JAMII KUTOKANA NA KUJIKITA KATIKA KUANDIKA HABARI TOFAUTI ZA UHAKIKA NA ZILIZOFANYIWA UCHAMBUZI WA KINA...........

Thursday, April 23, 2015

TASAF: USHIRIKI WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUELIMISHA UMMA JUU YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI

Ni Mtaalam wa Mawasiliano kutoka Makao makuu ya TASAF Zuhura Mdungi akitoa mada ya Mkakati wa mawasiliano wa TASAF na uwekaji wa kumbukumbu

UPOTOSHWAJI wa habari kwa makusudi kwa kutolewa ujumbe ambao siyo sahihi kuhusu mpango wa kunusuru kaya masikini nchini  ni miongozi mwa changamoto kuhusu mpango wa kunusuru kaya masikini.

Hayo yamebainishwa na mtaalam wa mawasiliano kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Zuhura Mdungi wakti akitoa mada juu ya mkakati wa  mawasiliano ya TASAF na uwekaji wa kumbukumbu katika kikao kazi cha waratibu maafisa ushauri na usimamizi na waandishi wa habari wa mikoa ya Shinyanga, Kagera na Geita kinachofanyika jijini Mwanza.
Baadhi ya waandishi wa habari wanashiriki kikao kazi cha waratibu wa mpango maafisa ushauri na wasimamizi na waandishi wa habari wa mikoa ya Shinyanga, Kagera na Geita

Zuhura amesema kuwa kumekuwepo na utoaji wa habari amabzo jamii inazipokea hujikuta wakishindwa kuwa na uhakika kutokana na utaratibu ambao umewekwa katika harakati za mpango wa kunusu kaya masikini.

Aidha amesema kutowafikia walengwa habari kwa wakati nalo limekuwa ni tatizo lingine.

Ameongeza kuwa yapo mambo ya kuzingatia katika kuendelea kutoa taarifa sahihi mpango na kurekebisha taarifa mara inapotopkea kama upotoshaji wa habari.


Amesema kuwa ni vema wakashirikishwa wataalam wakati wa kutoa maelezo ya kitaalam ili taarifa zinazotolewa ziwe sahihi zisizo za upotoshwaji.

Akizungumzia wajibu wa Menejimenti ya Mfuko wa maendeleo ya Jamii TASAF mtaalam huyo wa mawasiliano amesema ni kujenga uelewa wa pamoja kwa wadau wote kwa kutumia njia mbalimbali.

Pia ni kuwawezesha upatikanaji wa taarifa muhimu kuhusu mpango katika ngazi ya jamii.

No comments:

Post a Comment