Hayo yamebainishwa na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la HelpAge International Tanzania,
Smart Daniel wakati akifungua mkutano wa wadau
wanaojihusisha na kulinda na kutetea haki za wazee nchini, wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari unaoendelea jijini Dar es
Salaam
Mkurugenzi huyo amesema kuwa kutokana na hali hiyo ipo haja ya kufanya jitihada za maksudi za kuhakikisha sera ya wazee ya mwaka 2003 inatungiwa sheria ili wazee hapa nchini waweze kutambuliwa kisheria vinginevyo wazee wataendelea kukabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya ukosefu wa huduma bora za Afya
Ameongeza kuwa hii ni kutokana na
ukweli kwamba hivi sasa kuna
zaidi ya wazee Milioni Mbili na Nusu nchini
idadi ambayo inazidi kuongezeka kila kukicha wakati hakuna mipango yoyote yenye tija kwa
wazee hao
Aidha Daniel ameelezea
idadi ya watu duniani waliopo hivi sasa
na katika kipindi cha miaka 35
ijayo huku akitolea mfano nchi ya Japan
ambayo imeweza kujipanga vizuri katika kuwashughulikia wazee ambapo zaidi ya
asilimia 30 wanahudumiwa kikamilifu ikilinganishwa na hapa nchini asilimia nne
wapo katika mifuko ya hifadhi ya jamii
Akizungumzia suala la afya kwa wazee Afisa
Miradi ya Afya na Uwezeshaji wa kipato kwa wazee wa shirika la HelpAge International Leonard Ndamugoba amesema kuwa
bado huduma ya afya kwa wazee ni
tatizo huku mratibu wa kitengo cha Haki na Sheria kutoka HelpAge Joseph Mbasha amesema takwimu za mauaji ya wazee zinazidi kuongeka
Baadhi ya wadau na waandishi wa habari
katika mkutano huo wamesema kuwa changamoto zinazowakabili wazee zipo katika maeneo mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara ambayo ni kwazo kwa wazee katika kupata huduma za afya
Kwa upande wake mdau kutoka Shirika la MAPERECE la wilayani Magu mkoani Mwanza Julius Mwengela amesema kuwa licha ya changamoto hizo zipo jitihada zinazofanywa na shirika lake pamoja na jeshi la Polisi mkoani humo kwa kutoa elimu kwa waganga wa jadi
Naye mwandishi wa habari wa Star Tv na Radio Free Afrika mkoani Ruvuma Adam Nindi amesema kuwa waandishi wa habari wanaowajibu wa kuandika habari zinazohusu wazee kwani wao ni sehemu ya jamii
Mkutano huo umewashirikisha wadau wanaojihusisha na kulinda na kutetea
haki za wazee , waandishi wa habari
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini na maafisa ustawi wa Jamii wa wilaya na vijiji
na umeandaliwa na Shirika la Help Age
International
Mwisho
*********************************
No comments:
Post a Comment