MWAUWASA BODI
Na Wilson Elisha
Mwanza
Zaidi ya kiasi cha shilingi Milioni mia saba zinaendelea kutumika kwa ajili ya
kunusuru kero ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi waishio katika maeneo ya mlimani
jijini Mwazna
Hii itasaidia miundo mbinu
inayojngwa kuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho katika kutatua changamoto zinazowakbili
wananchi wa maeneo mbalimbali
Ni moja ya ziara ya wajumbe
wa bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya
Maji safi na usafi wa Mazingira jijini Mwanza MWAUWASA ya kukagua miradi ya
maji inayotekelezwa
Mkurugenzi mtendaji
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa mazingira MWAUWASA
Mhandisi Anthon Sanga amesema
kuwa licha ya changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama jijini Mwanza lakini zipo jitihada
zinazofanywa
Mhandisi Sanga amesema kuwa kutokana na kuanza
kujengwa kwa miradi ya dharura ya kunusuru hali ya upatikanaji wa maji anamini katika kipindi cha mwezi mmoja
kuanzia sasa wananchi waishio katika maeneo ya mlimani wataanza kunufaika na
mradi huo
Mwakilishi wa Wizara ya
Maji ambaye ni Mjumbe wa bodi ya maji jijini Mwanza MWAUWASA Mhandisi Paschal
Hamuli amesema kuwa serikali itaendelea na jitihada za kuhakikisha wananchi
wanapata maji safi na salama ili kuondoa kero inayowakabili
Baadhi ya wajumbe wa bodi
ya maji MWAUWASA ambao wamejionea hali halisi ya namna ambavyo ujenzi wa miundombinu ya maji
unavyoendelea hawakusita kuelezea furaha yao licha ya changamoto zilizopo
Katika kutatua kero ya
maji kwa wananchi Mamlaka ya Maji safi
na usafi wa mazingira jijini Mwanza MWAUWASA
wameanzisha miradi ya dharura kwa kuweka pampu ya kusukuma maji kwenda
katika baadhi ya maeneo
Mwisho
************************************************
No comments:
Post a Comment