Licha ya maeneo mengi nchini Tanzania kuzungukwa na
vyanzo vya maji,bado maeneo hayo yanatajwa kukabiliwa na uhaba wa maji hasa
wanaoishi maeneo ya milima na miinuko,
Hata hivyo jukumu la
serikali linatajwa kuhakikisha maeneo hayo yanapatiwa huduma ya maji safi na
salama kwa kuzingatia malengo ya meliniamu ya kuhakikisha maeneo ya mjini
yanapatiwa huduma hiyo kwa asilimia 95 na vijijini asilimia 85 ifikapo mwaka
2020.
Jiji la Mwanza ni moja ya
maeneo yanayokabiliwa na matatizo ya upatikanaji wa maji safi na salama hasa
katika meneeo yenye milima na miinuko
Kutokana na changamoto
hiyo inayowakabili wananchi Naibu katibu
mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Ngosi
Mwihava amefanya ziara ya kutembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa na Mamlaka
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza MWAUWASA
Eneo la Isamilo na mji
mwema ni kati ya maeneo yaliyopo milimani ambayo yamekuwa yakikabiliwa na uhaba wa maji kwa
muda mrefu sasa ni mwanzo wa maisha mapya ya
furaha kupata maji yaliyo safi na salama.
Mhandisi Anthony Sanga ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa MWAUWASA na Mhandisi
Abbas Muslim Meneja mradi MWAUWASA wamesema kuwa miradi yote inayotekelezwa
na MWAUWASA ina lenga kutataua uhaba wa ,maji kwa kipindi kifupi ingawa upo mradi mkubwa ambao unatarajiwa kutataua kero hiyo katika maeneo mengi
Hata hivyo Wabunge wa
majimbo ya Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza Angelina Mabula na Stanslaus
Mabula wameiomba serikali kuisaidia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira jijini Mwanza MWAUWASA ili iweze kuondoa kero ya upatikanai wa maji
safi na salama inayowakabili wananchi
Naibu katibu Mkuu wa
Wizara ya Maji Mhandisi Ngosi Mwihava amefafanua hoja za wabunge hao kuwa serikali inatambua mbali ya
kuwa maji ni uhai pia ni sehemu
ya uchumi hivyo suala hilo litafanyiwa kazi kadri
itakavyowezekana
Ziara hiyo ya Naibu katibu
mkuu wa Wizara ya Maji imehitimishwa kwa
kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano
ya mkopo wa fedha za utekelezaji wa miradi ya maji inayofadhiliwa na Benki ya
maendeleo ya Ujeruman KFW
Mwisho
**************************
No comments:
Post a Comment