Mratibu wa kambi ya macho kutoka Taasisi ya Bilal Muslim nchini Tanzania Ain Ashaff alielezea juu ya matibabu hayo kwa wagonjwa wa macho
Wakati idadi ya wagonjwa wa macho nchini ikizidi kuongezeka kila kukicha zimetajwa sababu mbali mbali ikiwemo chakula huku zaidi ya wagonjwa 300 wenye
matatizo hayo mkoani Mwanza wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa macho kati
ya wagonjwa 5000 watakaopatiwa matibabu hayo
na Taasisi ya Bilali Musilim Mission ya nchini Tanzania.
Matibabu hayo yanayotolewa na jopo la madaktari bingwa wa huduma za
upasuaji wa magonjwa ya macho ni ishara tosha kuwa ni mkombozi wa
utatuzi wa magonjwa hayo ambayo imekuwa
ni changamoto kubwa miongoni mwa jamii kutokana na kuwa na gharama kubwa.
Mwandishi Wilson Elisha ameandaa taarifa ifuatayo
Mzee Philimon Bashigwa
mkazi wa Mkuyuni jijini Mwanza mwenye umri wa miaka 78 akiwa ni mmoja wananchi
ambao wamefika kupata matibabu ya macho lakini yeye anasema huduma hiyo imefika
mda mwafaka.
SB: Mzee Philimon Bashigwa – Makazi wa Mkuyuni
Baadhi ya wananchi
waliofika katika klinki hii ya macho kwa ajili ya kupata matibabu huku kundi
kubwa wakiwa ni wazee na wanawake wanaonekana kujitokeza kwa wingi.
Madaktari bingwa waliobobea
katika suala la upasuaji macho
wakiwajibika katika majukumu yao ili kufaniksha matibabu kwa wagonjwa wa macho.
Mratibu wa kambi ya macho
kutoka Taasissi ya Bilal Muslim Misheni ya nchini Tanzania Ain sharif akiongea wakati
wa zoezi la upimaji amesema kuwa lengo ni kuona watanzani wanaondokana na
tatizo hilo.
SB: Ain Shariff Mratibu Kambi ya Macho Bilal Muslim
Tanzania
Aidha Shariff amesema kuwa
uapasuaji matibabu pamoja na dawa wanatoa bure japo kuwa wagonjwa wa upasuaji wanapelekwa
katika Hospitali ya Sekoutoure hivyo wakazi wa jiji la Mwanza amewataka kutumia
fursa ya uwepo wa madaktari bingwa kijitokeza kwa wingi
SB: Ain Shariff - Mratibu Kambi ya Macho Bilal Muslim Tanzania
Baadhi ya watu
waliojitokeza kupata huduma hiyo ya macho wameiomba Taasisi hiyo kujenga utamaduni
wa kutoa huduma hiyo ili kusaidia watu
wengi zaidi ambao wanasumbuliwa na ugonjwa wa macho
VOX 3
1.Mosses Messo -
Mgonjwa wa macho
2.Verediana Kileo – mgonjwa wa macho
3.Aman Abdallah
- Mgongwa wa macho
Taasisi ya Bilali Musilim
misheni Nchini imekuwa ikishirikiana na taasisi za serikali katika kuihudumia
jamii ili kukabiliana changamoto mbali mbali za kujiletea maendeleo
Taasisi hiyo imeshafikia
baadh ya mikoa hapa nchi katika kutoa huduma ya macho kwa wagonjwa na hivyo
huwawezesha wenye matatizo ya kutoona kuweza kuona.
Mwisho
***************
No comments:
Post a Comment